Monday, 17 October 2016



SOMO: KUTOKA
UTANGULIZI
Kutoka ni kuhama kutoka nafasi ya chini au kutokuwepo mazingira ya kwanza kwenda mbele. Mfano unaweza kwenda kwa mtu au kwa rafiki yako usipomkuta utaamua kuulizia aliko watu watakujibu unayemtafuta hayupo katoka,maana yake mazingira hayo hayupo.
Nilipokuwa ninasoma habariza wana wa Israeli walipokuwa wako utumwani Misri Mungu baada ya kuwaona wanateseka sana kwa kutumikishwa na Wamisri aliandaa mpangowakuwatoa Inchi ya Misri ilikuwapeleka Inchi ya ahadi. Si rahisi kuelewa hali hii lakini pia mtumishi wa Mungu IBRAHIM  Mungu alipotaka kumuinua na kumbariki awe taifa kubwa ambacho Mungua likifanya nikumwambia atoke katika Nchi ya baba yake na jamaa yake ili aende mahali atakapo ambiwa na Mungu, hiyo haitoshi baada ya Yesu kuja Duniani kwa mpango wa kumwokoa mwanadamua liwakuta kina Petro wakivua samakia lichokifanya nikuwatoa kwenye uvuvi wa samaki kuwaandaa ili wawe wavuvi wa watu. Swali je kwa nini Yesu asingewapa maagizo ya kuhubiri mpaka awatoe mahali walipokuwa ndipo aweze kuwapa maagizo? Au kwanini Abraham hakubarikiwa mpaka alipotoka kwenye Nchi ile? Kumbe tunagundua kutoka ni kwamuhimu kwa kila mtu. Fikilia juu ya mtoto anapozaliwa anabebwa kwa kuhurumiwa hata aliyembeba anadhani animuumiza lakini unafikia wakati ambao mtoto atakaa mwenyewe, ataanza kutambaa. Kusimama, Kutembea hatimaye kukimbia hizo zote ni hatua za kutoka kwa mtu.

KWA NINI TUNAPASWA KUTOKA
Kwa nini tunapaswa kutoka?
1.Kwasababu ni mpango wa Mungu. Ili Mungu afanye kazi na mtu lazima amtoe kwenye mazingira aliyomo, ndipo anapoanza kumtumia kwa mfano ukitizama katika maandiko matakatifu katika kitabu cha wakolosai inaeleza waziwazi juu ya swala hili la mtu kutoka katika mazingira au mahali Fulani ili Mungu amtumie vile apendavyo.
Kol 1:13 ( naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa mwana wa pendo lake.)
Mfano mzuri tuna uona kwa Abraham mwanzo 12:1-2 kabla Mungu hajambariki sharti la kwanza alilompa alimwambia atoke kwao mahali pa wazazi wake na ndipo alipoanza kusema naye baada ya kutoka.

2.Ili kuliondoa tegemeo letu kwa watu au kwa vitu badala yake tumtegemee Mungu Yer 17:5b amelaaniwa mtu Yule amtegemeaye mwanadamu kusudi la Mungu kumtoa Abraham kwenye nyumba ya baba yake na ya jamaa zake ilikuwa ni kulivunja tegemeo la Abraham kwa wazazi wake na ndugu zake .


Pointi ya msingi kijana anapokuwa yungali kwa baba yake na mama yake anakula, anavishwa na kila kitu akiomba anapewa hawezi kuwa na mwamko wa kimaisha wa kutafuta vya kwake maana tegemeo lake lingalopo kwa wazazi wake na ndugu zake na mara nyingi vijana wa namna hii hujikuta wakitumia muda wao vijiweni na vijana wa makundi lika na mwisho kuondokewa na wito wa kiutumishi na kuonekana mzigo kwa wazazi wao na ndugu zao hadi imepelekea wazazi wao kuwafukuza nyumbani ili waweze kujitegemea.

ILI UTOKE LAZIMA UYACHOKE MAZINGIRA ULIYOPO
Mara nyingi kutokuyachoka mazingira kumewafanya  watu wengi washindwe kutoka mahali walipo mfano huwezi kujenga nyumba au kutoka kwenye upangaji kama mazingira ya upangaji hayajakuchosha, wapo watu si kwamba hawana pesa za kuweza kujenga kwao na bado wako katika upangaji, hao mazingira ya upangaji hayajawachosha.

Pia wapo watu wameshindwa kumtumikia Mungu kwa wito aliowaitia kwa sababu bado wanapenda  kuwa washilika kwa hiyo wanajihesabu bado watoto yer 1:6 yeremia alisema hawezi kuifanya kazi ya bwana kwa sababu yeye ni motto.
Kutamani ya kwako mwenyewe hata kama umeajiliwa kwenye kampuni, ofisini au dereva wa daladala nk. Kama hujatamani kuona kwamba unafanya kazi yako mwenyewe hauwezi kutoka hapo, tuanmwona yakobo katika mwanzo30:30c alipomtumikia mjomba yake ilifika kipindi alipomwambia nilini nitaangalia mambo yangu mwenyewe.

Musa alipokuwa mtu mzima alikataa kuitwa mwana wa binti farao ebr 11:24, kuna hali zingine haziondoki maishani mwa mtu mpaka ajitambue yeye ni nani na achukue hatua za kukataa hali hiyo kwa jina la Yesu ndipo aweze kutoka. Shida inakuja kwa mtu asiyejitambua itakuwa kwake vigumu kutoka mahali alipokwenda mahali pengine.
Mungu anapotaka kukutumia haangalii sababu  za wewe kutokutoka hapo ulipo na kwenda katika nafasi au daraja ambalo anataka utumike ili kulitimiza kusudi lake mfano mzuri ni wakati Yeremia anaitwa na Mungu ili aweze kulitimiza kusudi la Mungu alijitetea kuwa ana umri mdogo lakini Bwana hakuangalia umri au sababu za Yeremia alichokiangalia ni Yeremia kutimiza kusudi la Mungu yer 1:6-7

Ili utoke ni lazima kuyaacha mambo Fulani uliyoyazoea Daudi aliambiwa kuviacha vyombo alivyokuwa navyo ili aweze kulitimiza kusudi la Israeli 1 samweli 17:20,22

Kuna watu wameshindwa kuitikia kwenye kusudi  kwa sababu ya kutokuacha yale waliyokuwa wameyazoea. Mfano mke wa ruthu kilichomfanya abaki pale na kuwa nguzo ya chumvi ni kwa sababu ya maisha  yaanasa aliyokuwa ameyazoea mwanzo 19:26.



KUUJUA WAKATI WAKO
Mhubiri 3:1 kwa kila jambo kuna majira yake na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu. Onyo usitoke kama wakati wako bado lakini pia usipishane na wakati wako utakuja kuutafuta hauta upata tena maana utakuwa ni wakati wa wengine.

Mfano msichana akishindwa kuujua wakati wa kuolewa atakuwa anatoa majibu kwa wachumba wanao kuja  kumchumbia kwamba Mungu hajasema nae kwanini?
1.Anajiona mtoto
2.kutojua kuwa ni wakati wake
3.Kuwalinganisha wachumba wanakuja kumchumbia
i)Elimu
ii)Mwonekano
iii)Mali
Vitu hivi vimewafanya wasichana wengi kupishana na wakati wa kuolewa, si kwamba ambao wametimiza umri wakuolewa lakini hawaolewi si kwamba hawajawahi kuchumbiwa lakini walichengana na wakati hawakujitambua au kujua wakati wao.

Huwezi kupishana na wakati wako ukaja kupata kivyepesi mpaka ujute. Ombi langu baada ya kulisoma somo hili Mungu akupe macho ya kuona wakati wako kwa jina la YESU; ubarikiwe na Bwana AMEN.
Imetayarishwa na Mwl MUSSA FESTO
Kwa ushauri au mashauri wasiliana kwa namba hii.
0675415262

No comments:

Post a Comment